Katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa kila siku ya jumatatu saa 3:30, mkongwe wa bongo fleva nchini kutoka kundi la East Coast Team GK amesema wasanii wengi nchini wanatumiwa na wanasiasa kama toilet paper jambo linalochangia kushusha hadhi ya wasanii na industry nzima ya sanaa hiyo.
Amesema pamoja na bongo fleva kukua kwa kiwango kikubwa tofauti na kipindi cha nyuma na kupata mwitikio chanya kwenye jamii, bado suala la kutumika vibaya wakati wa uchaguzi ni changamoto mojawapo.
Mytake: nadhani ni vema wasanii wakajikita kuhimiza utaifa zaidi na kipindi hichi cha uchaguzi watunge nyimbo za kuelimisha jamii kuhusu uchaguzi na maendeleo yao kwa ujumla. Is this an awkward mind or wise thinking? Unadhani kuna haja ya msanii kuonesha hadharani mrengo wake kisiasa
22 Jan 2015
New