Vijimambo:Jokate Achekelea Kumbwaga Lulu Kwenye Nani Mkali - MULO ENTERTAINER

Latest

22 Jan 2015

Vijimambo:Jokate Achekelea Kumbwaga Lulu Kwenye Nani Mkali

Mwanamitindo namuigizaji wa filamu , Jokate Mwegelo  ameibuka mshindi kwa urembo na muonekano katika picha zinazoonekana mitandaoni nchini na kumbwaga aliekuwa mshindani wake ,Elizabeth Michael ‘Lulu”.

Kwa mujibu wa GPL, mtandao mmoja wa hapa nchini umeendesha zoezi la kuweka picha zao kali zinazowaonesha wote wawili wakiwa na muonekano na picha kali huku wakiuliza nani zaidi ya mwenzake.Jokate ameibuka mshindi kwa kupigiwa kura tano huku watu wakimsifia kuwa ni wa kimataifa zaidi ambapo Lulu alionekana kupigiwa kura na mtu mmoja.

Akizungumzia  ushindi huo Jokate  aliwashukuru Watanzania kwa kumpenda na kumpa nafasi lakini aliwasihi kwa kuwaambia kuwa yeye aonavyo wote ni warembo.“Mimi naona sisi wote ni warembo, nawashukuru Watanzania walionichagua na kuniona nafaa,” alisema Jokate
Lulu alipotafutwa, hakupatikana