Siku za hivi karibuni kumeibuka na mtindo mpya wa watu kulishana keki wa kutumia mdomo yaani “Kudendeka”.
Picha ya mrembo na mwigizaji wa filamu Wema Sepetu akilishwa keki kwa mdomo na dada yake Diamond, Esma imeibua mjadala mtandaoni baada ya baadhi ya watu kudai kuwa Wema anataka kumrusha roho Zari ambae awari aliandika ujumbe mtandaoni na kumuita Esma WIFI. Huku wengine wakiona kama ni kawaida kwani kwa kiasi kikubwa Wema ndio aliewawezesha Esma na Petti Man wakafunga ndoa.
Tukio hilo lilifanyika hivi majuzi, kwenye Birthday Party ya Esma iliyofanyika Samaki Samaki, Masaki.
Mastaa kadhaa wa hapa Bongo walitokea kwenye pati hiyo wakiwemo, Aunty Ezekiel, Queen Dorleen,Mirror na wengine wengi.
5 Feb 2015
New