Jack Wolper: Naijua Thamani Yangu Siko Tayari Kutumika na Wafanya Biashara Bure - MULO ENTERTAINER

Latest

8 Mar 2015

Jack Wolper: Naijua Thamani Yangu Siko Tayari Kutumika na Wafanya Biashara Bure


Mrembo na staa wa Bongo Movies ,Jaqueline  Massawe Wolper  amefunguka kuwa anajua thamani yake kama msanii hivyo hawezi kutumika na wafanyabiashara kwa kuwatangazia biashara zao bila kuwa na mikataba ya kueleweka au mtu kumfanyia maamuzi pasipokuwa na makubaliano na kufikia mwafaka kuhusu hilo.
“Kujenga jina katika sanaa si kazi ndogo, unapigana na kujitoa na inapotokea maarufu watu wanaanza kuona thamani ya jina ulilolijenga basi ni wakati wa kulilipia na si bure tena,”anasema.
Jack anasema hivi karibuni alikataa kupiga picha na kampuni moja baada ya kutaka apige picha akiwa ameshika bidhaa mkono wakimlaghai kuwa wamemletea zawadi pia wakitaka picha za bidhaa hiyo atumie katika akaunti yake ya kijamii, anajua walifanya hivyo kwa sababu ana watu wengi, lakini yeye alikataa.