Kajala Masanja Aibiwa Nguo ya Ndani Kiuchawi......Aikuta Nje Ikiwa Imelowa Damu - MULO ENTERTAINER

Latest

17 Apr 2015

Kajala Masanja Aibiwa Nguo ya Ndani Kiuchawi......Aikuta Nje Ikiwa Imelowa Damu

Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’ amepatwa na dhahama ya aina yake baada ya kuibiwa nguo yake ya ndani kimazingara kisha kuikuta nje ikiwa imeloa damu.

Kwa mujibu wa Gpl , mara nyingi Kajala ana kawaida ya kufua na kuzianika nguo hizo ndani lakini katika mazingira ya kutatanisha moja ilipotea na kila alipofanya jitihada za kuitafuta, hakuiona.

Baada ya nguo hiyo kutooneka ghafla, Kajala alichanganyikiwa sababu nyumbani kwake hakuna hata panya ambaye anaweza kuibeba pengine na kuitupa sehemu nyingine.

Habari  zinaarifu kuwa baada ya kulitafuta ‘kufuri’ hilo kwa muda mrefu bila mafanikio, alikuja kulikuta kwenye ndoo tupu ya maji tena ikiwa imetobolewa huku ikiwa imetapakaa damu.