Kajala Amrushia Ujumbe Wema Sepetu Ambae Amekuwa Mgumu Kusamehe “Love will save us” - MULO ENTERTAINER

Latest

17 May 2015

Kajala Amrushia Ujumbe Wema Sepetu Ambae Amekuwa Mgumu Kusamehe “Love will save us”

Brigthon Masalu
KAJALA Masanja ambaye ana bifu na aliyekuwa shosti wake mkubwa, Wema Sepetu ‘Madam’ amedaiwa kumpa rafiki yake huyo wa zamani ujumbe unaoashiria upendo kwa kuvaa gauni lenye maandishi yaliyosomeka “Love will save us” yakimaanisha upendo utatuokoa.

‘Katukio’ hako kalinaswa na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa New Maisha, Masaki jijini Dar kulikokuwa na onesho la Mrs. Mabeste Charity (mke wa msanii Mabeste) ambayo ilikusanya wasanii wengi wakiwemo Kajala na Wema.

Baada ya mwandishi wetu kushuhudia ujumbe huo mgongoni mwa Kajala huku marafiki zake wakidai ni maalum kwa Wema ambaye amekuwa mzito kusamehe ugomvi wao, alimuuliza kama amemlenga Wema au ni vazi tu alivaa?
“Jamani mimi nimevaa tu, sikumkusudia mtu,” alisema Kajala.Wema na Kajala wamekuwa kwenye bifu la kuchukuliana bwana na bado hawajafikia muafaka.