Majambazi Wakamatwa Wakitaka Kuiba Katika Benki ya NMB Tawi la Sinza Mori-Dar - MULO ENTERTAINER

Latest

19 May 2015

Majambazi Wakamatwa Wakitaka Kuiba Katika Benki ya NMB Tawi la Sinza Mori-Dar

Polisi jijini Dar wamewakamata watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa katika jaribio la kuiba pesa katika benki ya NMB iliyopo Sinza-Mori, Dar.

Tukio hilo limetokea mchana wa leo katika Benki ya NMB tawi la Sinza-Mori jijini Dar ambapo majambazi hao walikamatwa wakiwa katika harakati za kutekeleza tukio hilo.

Majambazi hao baada ya kukamatwa wamepelekwa katika kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama jijini Dar.