Shirikisho la Mpira Duniani Fifa Lachafuka Tena..Maafisa Sita Wakamatwa Kwa Rushwa - MULO ENTERTAINER

Latest

28 May 2015

Shirikisho la Mpira Duniani Fifa Lachafuka Tena..Maafisa Sita Wakamatwa Kwa Rushwa

Maofisa sita wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) wamekamatwa jijini Zurich kwa tuhuma za rushwa.

Maofisa hao akiwemo Makamu wa Rais wa Fifa, Jeffrey Webb wametiwa nguvuni na Jeshi la Polisi la Uswis, leo saa 12 alfajiri.

Maofisa hao walikamatwa katika hoteli moja ya kifahari na kutolewa huku wakiwa wamefunikwa kwa shuka na wafanyakazi wa hoteli hiyo ili wasipigwe picha.

Inaelezwa wanatuhumiwa kupokea rushwa ili kutoa nafasi kwa mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi na 2022 yatakayofanyika nchini Qatar kufanyika katika nchi hizo.

Pia imeelezwa memba wengine 10 wa kamati ya utendaji ya Fifa watahojiwa.

Madai hayo yameongeza kwamba maofisa hao wanaaminika kuchota rushwa hadi ya dola milioni 100 kwa ajili ya kuizipa nchi hizo nafasi.

Msemaji wa Fifa, Walter de Gregorio amesema licha ya maofisa hao kutiwa mbaroni, komgamano la kesho Ijumaa kuhusiana na uchaguzi wa Rais wa Fifa litaendelea kama kawaida.

Rais wa sasa wa Fifa, Sepp Blatter ndiye anayepewa nafasi kubwa kushinda kwa muhula wa tano mfululizo.