Bongo Star Search ni Janga la kitaifa...Mchakato Umejaa Dharau, Kejeli na Kukatishana Tamaa - MULO ENTERTAINER

Latest

17 Aug 2015

Bongo Star Search ni Janga la kitaifa...Mchakato Umejaa Dharau, Kejeli na Kukatishana Tamaa

Kwa mtu yeyote intellectual ambaye huwa anatazama Bongo Star Search atakubaliana nami kuwa mchakato huo wa kusaka mwanamuziki bora mwenye kipaji umejaa dharau,kejeli na kukatisha tamaa,hawa Master Jay na Salama Jabir ni majaji feki kabisa wanaowakatisha tamaa vijana wenye vipaji,namsifu sana Madam Rita, dada huyu hajawahi kumkatisha tamaa mshiriki yoyote,hata anapoonekana kushindwa yeye humtia moyo ama kukaa kimya,lakini salama na master jay huwatolea maneno ya kejeli,vijana wangu wa Tanzania wenye vipaji mbalimbali msikatishwe tamaa na hizi taasisi za kihuni zinazojifanya zina uwezo wa kubaini vipaji vyenu,leo hii Diamond, Lady Jay Dee, Prof Jay, Dully sykes na wengineo wangeenda kutafuta vipaji vyao Bongo Star Search wangerudi wakiwa wamekata tamaa kwa kukutana na kina Master jay na Salama, simameni wenyewe achaneni na hawa wahuni, mtapoteza vipaji vyenu bure, historia inaonyesha kuwa, hakuna mtu aliyefanikiwa maishani kwa kuwekwa katika mizani ya ushindani bali alifanikiwa kwa kujituma mwenyewe akiamini atafanikiwa