Rais Kikwete Atua mjini Dodoma Kuendesha Vikao vya Chama cha Mapinduzi - MULO ENTERTAINER

Latest

11 Aug 2015

Rais Kikwete Atua mjini Dodoma Kuendesha Vikao vya Chama cha Mapinduzi

Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo ataongoza vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati kuu ya CCM vitakavyofanyika katika ukumbi wa White House Makao Makuu Dodoma.
 
Alhaj Kimbisa amekanusha uvumi uliosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa ameihama CCM. Kushoto ni Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana

Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na KAtibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahmana Kinana baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo ataongoza vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati kuu ya CCM vitakavyofanyika katika ukumbi wa White House Makao Makuu Dodoma.