Tajiri huyo anayetambulika kwa jina la Nassoro Ahmed bin Slum anayemiliki kampuni ya Bin-slum Tyres Ltd, amejitokeza na kukiri kumiliki baadhi ya makontena yaliyokumbwa na kashfa hiyo lakini amekana kosa lenye sura ya kukwepa kodi akidai kuwa limefanywa na wakala wake.
“Wafanyabiashara hatuna mamlaka ya kulipa kodi moja kwa moja serikalini. Tunalipa kodi kupitia kwa wakala aliyechaguliwa na serikali. Mimi nilimlipa kazi wakala wangu ambaye nimekuwa nikifanya naye kazi kwa miaka 10,” Bin Slum ameliambia gazeti la Raia Mwema.
“Mara kwa mara huwa ananiletea nyaraka za malipo ya kodi lakini kwenye mzigo huu wa sasa ambao kontena zangu zina matatizo ya kodi, alinitangulizia mzigo na mimi nikamdai nyaraka. Yeye aliniambia ananiandalia faili,” alieleza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliagiza wote wanaohusika na kashfa hiyo kukamatwa na kuchukuliwa hatua na kodi iliyokwepwa ilipwe.
Tayari watu 12 wanashikiliwa na jeshi la polisi kufuatia sakata hilo.