WASTARA Atoa Kali ya Mwaka Huu...Adai Nahisi Mauti yapo Karibu yake..... - MULO ENTERTAINER

Latest

2 Jan 2016

WASTARA Atoa Kali ya Mwaka Huu...Adai Nahisi Mauti yapo Karibu yake.....

Ikiwa leo ni mwaka wa tatu toka msanii wa filamu, Sajuki Juma afariki dunia, mke wake Wastara Juma ameendelea kupitia mitihani mbalimbali ya maisha hali inayomfanya aombe Watanzania wamuombee dua.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wastara ameandika.

Naanza kwa kumshukuru mungu wangu anaenipa pumzi ya bule mpaka mda huu. Sina budi kusema haya nitakayoyasema kwa ajili mwaka mpya unaonza. Ni miaka 4 na miezi 6 leo imetimia toka furaha yangu ilipoingia dosari.

Mungu alinipa mtu wa kunipa furaha kwa sababu kilakitu Alhamdulilah nilikuwanacho kulingana na nafasi yangu lakini sikuwa na furaha lakini furaha hiyo aikudumu nakumbuka ilikuwa mwezi 6/ 2011 marehemu Sajuki alipoanza kuumwa ndipo furaha ilipoanza kupotea kwa sababu sikupata nafuu wala moyo wangu kupumzika mpaka leo.

Nimejaribu kutafuta furaha kila sehemu kila njia ila imeshindikana na Mungu nae anaendelea kunipa mitihani ya maradhi ambayo naamini yatapona na kuisha soon ila kuishi katika mazingira hayo kwa mtu mwengine angekuwa kama kizee hata kuchana nywele ingekuwa shida ila katika maisha ya maumivu na Sajuki siku moja aliniambia mke wangu mi naumwa ila sipendi kukuona ukiwa mchafu na pia usinizuie kwenda kokote kwa sababu nitakufa siku yoyote tutumie muda uliobakia kufanya kile kitu moyo unataka.

Nami kwasasa naishi hivyo nahisi mauti yapo karibu yangu sana hivyo kile moyo wangu unataka ndicho nakifanya hta moyo ukiniambia inuka na maumivu yako nipelke baharin basi naupelka uko ukisema nipelke disco naupeleka uko ukisema nikakeshe msikitin naupeleka uko hivyo sitabariki na sipendi kuishi ili mtu anione nina maumivu nalazimisha furaha japo aipo hivyo mnisamehe wale wote msionielewa kokote mkinikuta mniche tu sifanyi kitu kumkera mtu i need realif ya moyo wangu maskin unanivuja damu kilasiku natamani nifanye lolte ili upumue hakuna kitu kibaya kma kupoteza furaha na tumain unaishi kma uko dunia ya peke yako nimeongea hya ili muelewe hisia zangu kuwa hta ukiongea kitu ambacho sijakifanya sihusiki au kunitafsiri vibaya naumia mara 2 nahisi kma na wew ni mmoja ya wale wasiopoenda kuona nikifurahia uwepo wangu duniani.

Viongozi wangu ndugu jamaa wasanii wenzengu na mshabiki wangu nawaomba kwa pamoja mpige goti kuniombea 2016 moyo wangu upate furaha ya kudumu upate dawa ya maumivu upate tabasamu la kweli na sio feki ninalotoa sasa aniondoshee maradhi yote moyo wangu unahitaji realif maskin mwaka 2016 uwe na neema kwetu sote amen.