“Uchaguzi wa Zanzibar utatuletea matatizo makubwa kitaifa tusipokuwa makini, hakuna namna yoyote katika bunge hili ya kutozungumzia suala la Zanzibar, iwapo matatizo ya Zanzibar yasipotatuliwa kwa makini, mpango huu hautatekelezeka”, alisema Saed Kubenea.Pia Saed Kubenea amesema watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini na mashirika m
balimbali ya kijamii yanaliona suala hilo, lakini wao kama wabunge hakuna ambaye amethubutu kuliongelea.
“Tunakaa kaa tu humu ndani, wakati maaskofu wanasema Zanzibar kuna tatizo, mashekhe wanaliona tatizo, tukajifanya hakuna matatizo, nchi yetu itafika pabaya na mpango wa maendeleo hautatekelezeka”, alisema Saed Kubenea