Kauli ya Makonda inavyoweza kutumika kama fursa kwa vijana wa Dar - MULO ENTERTAINER

Latest

25 Mar 2016

Kauli ya Makonda inavyoweza kutumika kama fursa kwa vijana wa Dar

Mkoa wa Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji yanayoongoza kwa uchafu Tanzania.

Siku chache zilizopita Rais Magufuli alifanya uteuzi wa wakuu wapya wa Mikoa, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda aliteuliwa kuwa mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam.

Baada ya uteuzi huo na kuapishwa ikulu, Makonda alifanya mkutano kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere ambao uliwajumuisha wenyeviti wote wa mkoa wa Dar es Salaam na wadau wengine wa maendeleo.

Agenda ya uchafu ndiyo ilishika nafasi kubwa kwenye mkutano huo. Mh Makonda aliwataka wenyeviti wote wa mkoa wa Dar es Salaam kuanza usafi kwenye mitaa yao, pia aliahidi kutoa zawadi ya gari lenye thamani ya shilingi milioni 20, na zawadi ya pikipiki kwa wajumbe wake ambao mitaa yao itaonekana ni misafi.

‘Kidole kimoja hakivunji chawa’, ushirikiano pekee na umoja ndiyo unaweza kufanikisha hili kutimia. Vijana wengi wapo mitaani wanalalamika hakuna ajira, lakini kwa hili inaweza ikawa neema na fursa pekee ya ajira kwao.

Vijana wanaweza kuunda vikundi vyao kwa ajili ya kufanya usafi kwenye mitaa yao na kuweka unlizi kwa pamoja, siamini kuwa kama kutakuwa na mwenye muda kila siku wa kufanya usafi na kumsimamia mwenzake kwenye hili.

Viongozi wa serikali za mitaa na wananchi wao wanaweza kupanga kuchangishana fedha fulani ili kuwapatia vijana hao ambao watakuwa wanafanya usafi na ulinzi kwenye mitaa yao. Hakuna kiongozi anayeweza kukutafutia kazi, ila anakutengenezea misingi ya kuweza kujiajiri mwenyewe kama hili lililotokea sasa.