Inabidi ujue Tanzania inao watu wenye pesa zao na wanayo malengo au mipango mikubwa zaidi ya kibiashara ambayo kama ikienda inavyotakiwa wanaweza kuifanya nchi hii kutajwa zaidi kuwa na matajiri miongoni mwa nchi zenye Mabilionea Afrika.
Kituo cha Television cha Marekani CNN kilimuhoji Mtanzania huyu na kikaweka kichwa cha habari ‘kutana na Bilionea mwenye umri mdogo Afrika‘ ni Mohammed Dewji ambaye ameajiri watu karibu elfu ishirini na nane kutokana na viwanda na biashara zake.
Mbunge huyu wa zamani wa Singida mjini amesema ‘nimekua nikitaka kununua Benki kwa miaka minne mitano iliyopita, sasa hivi nimeamua nataka kuanzisha Benki yangu kabisa japokuwa hii ishu ya Benki ya Barclays Afrika kuuzwa imekuja na nashawishika japo sijajua kama wanataka mnunuzi atakaeichukua Afrika nzima‘
‘Nimeshawishika kuinunua Barclays upande wa Afrika Mashariki na ninayo pesa tayari, sijajua wanaiuzaje lakini sina mpango wa kuichukua Barclays yote kwa Afrika, ningependa kuinunua upande wa Afrika Mashariki kwenye nchi za Kenya, Uganda, Tanzania yaani kwenye nchi nne au tano hivi’ – Mo
Dewji
March 24 2016 Mohammed Dewji aliandikwa na CNN kwamba anataka kuingia kwenye soko la ushindani Afrika na kushindana na Coca cola kupitia kinywaji chake cha Mo Cola na namnukuu akisema ‘tunashindana na Red Bull kupitia Mo Energy Drink’