Ni Marufuku Kuvaa Nguo Fupi Wilayani Siha Kilimanjaro, Sheria za Viboko na Faini zimetajwa - MULO ENTERTAINER

Latest

28 May 2016

Ni Marufuku Kuvaa Nguo Fupi Wilayani Siha Kilimanjaro, Sheria za Viboko na Faini zimetajwa

Moja ya matukio ambayo yanamake headlines katika Wilayani Siha Kilimanjaro ni pamoja na adhabu zinazotolewa kwa wale wanaovunja sheria, kingine ni kwamba kijiji cha Sanya Hoye kimepitisha adhabu ya faini ya Shilingi 50,000 pamoja na viboko 15 kwa atakayekutwa baa na mtoto mdogo au kuvaa nguo fupi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Sanya  Hoye, Moses Mnuo ametoa ufafanuzi wa maazimio waliyokubaliana katika kikao cha kijiji cha Sanya Hoye………

‘Tumepitisha sheria kwa mtu yeyote anayevaa nguo fupi kwa watoto wa kike ni marufuku tangu siku ile ya kikao kile, wanawake hao wanapotembea hapa usiku wana ajenda walizonazo wanafanya machafu yao kwa hiyo tutawapiga faini na hizo hela watapewa risiti’ Sikiliza Hapa