Dr. Cheni Aeleza Sababu za Kutojihusisha Tena na Filamu Nchini - MULO ENTERTAINER

Latest

5 Nov 2016

Dr. Cheni Aeleza Sababu za Kutojihusisha Tena na Filamu Nchini

Mwigizaji na mtayarishaji wa filamu nchini, Dr Cheni amesema hatatoa tena filamu nyingine kutokana na hali ya kibiashara ilivyo katika tasnia ya filamu hapa nchini

Dr. Cheni alisema hayo alipokuwa akizungumza na E News ya EATV ambapo alisema kuwa kazi zao hazina ulinzi na haiwafaidishi wasanii ndio maana huoni umuhimu wa kuendelea kutoa kazi hizo

Dr. Cheni alisema ukitoa leo filamu mpya baada ya siku moja utaikuta imesambaa nchi mzima ikiwa inauzwa tena kwa bei chee, alipoulizwa hadi lini ndo atatoa filamu, alisema kuwa hadi hapo Serikali itakapoingilia kutatua suala la kazi zao

"Siwezi kutoa tena filamu hadi Serikali itakapo hakikisha kuwa kazi zetu zipo salama, ukitoa filamu leo siku moja ya pili ya tatu unazikuta chini zinauzwa ambazo ni bandia, kilio chetu sisi bongo movie ni kazi zetu zinaibwa, namuomba Rais Magufuli aingilie kati suala hili kwani vijana wengi wamejiajiri kwenye bongo movie "alisema Dr Cheni