HANSCANA Aeleza Chanzo Cha Ajali Mbaya ya Gari Aliyopata Akiwa na Darassa - MULO ENTERTAINER

Latest

20 Dec 2016

HANSCANA Aeleza Chanzo Cha Ajali Mbaya ya Gari Aliyopata Akiwa na Darassa

Muongozaji wa video za muziki nchini, Hanscana amefunguka na kueleza nini kilitokea hadi wakapata ajali mbaya ya gari akiwa na rapa Darassa pamoja na watu wengine wawili.

Ajali hiyo ilitokea wakati wakiwa njiani wakitokea Kahama mkoani Shinyanga kwenda Kakola mkoani humo kwaajili ya show.

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Hanscana amedai hajui chanzo cha ajali hiyo huku akidai hata yeye anashangaa kwani walikuwa kwenye mwendo wa kawaida sana.

“Dereva alikuwa Darassa wakati tunapata ajali na kusema kweli tulikuwa kwenye mwendo wa kawaida sana, ghafla tukashangaa kuona gari ina serereka na kupinduka mara nne. Kwa hiyo ni ajali kama ajali nyingine sema sisi tunashangaa mazingira ya ajali lakini yote ya yote tunamshuru Mungu kwa sababu wote ni wazima,” alisema Hanscana.

Aliongeza, “Kwa sasa tunaangalia namna gani tunaweza kurudi Dar es salaam kwa sababu huku tuliko ni mbali sana na tulikuja kwa ajili ya show,”

Mastaa mbalimbali wametumia mitandao ya kijamii kuwapa pole.