Wasanii Wapaza Sauti Zao Kuhusu Kupotea Kwa Roma...Wataka Viongozi Wajitokeze - MULO ENTERTAINER

Latest

7 Apr 2017

Wasanii Wapaza Sauti Zao Kuhusu Kupotea Kwa Roma...Wataka Viongozi Wajitokeze


Wasanii kupitia kikao kilichofanyika leo Tongwe records wamepaza sauti na kutaka viongozi wa Mkoa walivalie njuga suala hilo

Wasanii hao wamesema kuwa watekaji hao walitamka wazi kuwa wanamtaka msanii Roma na producer wake na walipoona watajulikana ndipo walipoamua kuondoka na watu wote waliokuwepo ndani ya studio za Tongwe records siku hiyo ya alhamisi juzi. 

Aidha Babu Tale ambaye ni meneja wa wasanii kadhaa akiwemo Diamond amesema kuwa kwa hili kamwe hamuogopi Paul Makonda na amemtaka kumrejesha mara moja msanii mwenzao. 

Aidha Babu Tale amesema kuwa anashangaa kuona Paul Makonda yupo kimya juu ya hili huku yeye akiwa kama kiongozi mkuu wa ulinzi na usalama ndani ya Dar es Salaam.