Padri Mapunda: Wapinzani sio Maadui, Mfalme Suleimani Hakujifanya Mungu mtu. JPM ajifunze - MULO ENTERTAINER

Latest

9 Sept 2017

Padri Mapunda: Wapinzani sio Maadui, Mfalme Suleimani Hakujifanya Mungu mtu. JPM ajifunze

PADRI Baptiste Mapunda ametaka JPM kutambua kuwa bila majadiliano na viongozi wengine wa vyama vya siasa vya upinzani, hatma ya nchi itakuwa mbaya sana siku zijazo.

Akizungumza katika Kanisa Katoliki Manzese, jimbo kuu la Dar es Salaam, Padri Mapunda alisema Rais JPM awe na busara na kufuata mwenendo wa Mfalme Suleimani ambaye katika uongozi wake alikuwa akiomba muongozo kwa Mungu na hakujifanya Mungu mtu.

“Hata Mungu aliwahi kukosolewa na Nabii Musa pale alipotaka kuwaondoa Waisraeli, sembuse binadamu tunaoishi na kufa?" Amehoji Padri Mapunda.

Source:Jamii Forums