Gigy Money Mapenzi Moto moto na Mpenzi Wake Wamalizana Ugomvi Wao - MULO ENTERTAINER

Latest

15 Feb 2018

Gigy Money Mapenzi Moto moto na Mpenzi Wake Wamalizana Ugomvi Wao

Gigy Money Mapenzi Moto moto na Mpenzi Wake Wamalizana Ugomvi Wao


MWANADADA ambaye ni mwana-muziki na muuza sura kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’, hivi karibuni amefunguka kwamba, hana matatizo tena na baba wa mtoto wake mtarajiwa aitwaye Mo Jay, na kwamba kila kitu kwa sasa wamekwisha kiweka sawa ambacho kilikuwa kinawafanya wagombane mara kwa mara.

Akichonga na Showbiz Xtra, Gigy aliongeza kuwa, wawapo wawili ‘tafaruku’ ndogondogo huwa hazikosekani, jambo ambalo lilikuwa linajitokeza kwao, lakini kwa sasa kila kitu kipo sawa na hawana tatizo kabisa.

“Sina shida yoyote na mpenzi wangu kwa sasa, kila kitu kipo sawa na yakiwepo ya kuzun-gumza kama tuna matatizo nitazu-ngumza huko mbele, lakini kwa sasa hakuna tatizo lolote,” alisema Gigy.