Trump Atoka Kimapenzi na Nyota wa Filamu za Ngono Trump Atoka Kimapenzi na Nyota wa Filamu za Ngono - MULO ENTERTAINER

Latest

15 Feb 2018

Trump Atoka Kimapenzi na Nyota wa Filamu za Ngono Trump Atoka Kimapenzi na Nyota wa Filamu za Ngono

Image result for TRUMP
Wakili binafsi wa muda mrefu wa Rais wa Marekani Donald Trump amekiri kumlipa nyota wa filamu za ngono dola 130,000, mwaka 2016.

Hatua hiyo inajiri wakati vyombo vya habari vikisema kwamba, nyota huyo wa filamu za ngono kwa jina Stromy Daniels alilipwa katika makubaliano ya kutozungumzia uhusiano wao.

Mrembo huyo aliwahi kusema kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Rais Donald Trump mwaka 2011 katika mahojiano lakini Wakili huyo alidai Rais Trump alikana kuwepo kwa uhusiano wowote kati yao.

Katika mahojiano ya mwaka 2011 na jarida la InTouch , nyota huyo wa filamu za ngono, alisema, alianza uhusiano na Rais Trump 2006 baada ya Melania Trump kujifungua mwanawe Barron.

Ripoti hizo zilizuka mwezi Januari wakati jarida la Wall Street liliporipoti kwamba alilipwa ili kuficha makubaliano fulani kabla ya uchaguzi mkuu wa 2016 hatua iliyomzuia kuzungumzia madai hayo.