Unai Emery Kukabidiwa Mikoba ya Arsene Wenger - MULO ENTERTAINER

Latest

22 May 2018

Unai Emery Kukabidiwa Mikoba ya Arsene Wenger

Unai Emery Kukabidiwa Mikoba ya Arsene Wenger
Klabu ya Arsenal inatarajia kumtangaza wiki hii aliyekuwa meneja wa Paris Saint-Germain, Unai Emery kurithi mikoba ya Arsene Wenger.

Emery ambaye ameachana na klabu ya PSG mwanzoni mwa mwezi huu ameonekana katika Jiji la London hapo jana siku ya Jumatatu akifanya mazungumzo na the Gunners.

Kocha huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 46, ameongoza klabu ya Ufaransa inayoshiriki na nafasi yake kuchukuliwa na Thomas Tuchel.

Chanzo kimoja kilichopo karibu na mazungumzo hayo kimeeleza kuwa Emery ndiye mgombea pekee aliyepewa nafasi ya kurchukua mikoba ya Arsene Wenger.