Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Mji wa Ohio nchini Marekani unaohusiana na athari zinazosababishwa na kupiga picha Binafsi “Selfie” na kuweka kwenye mitandao tofauti umegundua tabia ya watu hao. Watu waliofanyiwa utafiti huu ni 800 na wenye umri kati ya miaka 18 na 40.
Utafiti umeonyesha kuwa wanaopenda kujipiga Selfie wakiwa peke yao wanakuwa na tabia ya "ubinafsi zaidi" na hawapendi kujichanganya na watu wengine wala kwenda sehemu zenye watu wengi mara nyingi.
Watu hao pia wana tabia ya kurekebisha “Edit” picha kabla hawajaiweka kwenye mtandao wanaotumia, pia watu hawa hutumia muda mwingi kuchunguza na kuchagua picha gan ni bora zaidi kuiweka.
We unayepiga Selfie ni kweli unatabia hizi ?
UMEICHEKI HII ? Picha ya Beyonce mtandaoni iliyozusha uvumi kuwa anaujauzito !