Mke wa Roma Ataja Mstari Unaomnyima Usingizi Katika Wimbo wa 'Zimbabwe’ - MULO ENTERTAINER

Latest

12 Aug 2017

Mke wa Roma Ataja Mstari Unaomnyima Usingizi Katika Wimbo wa 'Zimbabwe’

Mke wa Roma Ataja Mstari Unaomnyima Usingizi Katika Wimbo wa 'Zimbabwe’
Mke wa R.O.M.A ,Nancy au Mama Ivan  amefunguka mengi kuhusu masahiri yaliyomo kwenye  ngoma  mpya ya mume wake iliyotambulishwa hivi karibuni katika vyombo mbalimbali vya habari aliyoipa jina la ‘Zimbabwe’ 



Akifanya mahojiano maalum kupitia kipindi cha Exclusive Interview cha Global TV, mama Ivan ameutaja msitari unaomuumiza na kumnyima usingizi ni kuhusu mmoja wa wabunge aliyetamka hadharani bungeni kuwa msanii huyo amemtukana Mkuu.

Msitari wenyewe;

..Na kuna mbunge alisema eti nimemtukana Mkuu, atahukumiwa na mkono wa Mungu,…. kwanza lini na kwa nini? Mimi nimtukane Mjomba? Umepewa gari la wagonjwa mimi Tanga ananijengea bomba…!

“Huo ndiyo msitari ambao unaniumiza, nikikumbuka yule mbunge aliyesema muacheni atekwe, anamtukana Rais? Kiukweli R.O.M.A hajawahi kumtukana Rais, ameimba kitu kilichomtokea, kilichomgusa na kipo moyoni. Sisi tumemwachia Mungu, tunasali sana na Mungu ndiye atahukumu mwisho wa siku,” alisema Mama Ivan.

Mama Ivan ameshukuru namna wimbo huo ulivyopokelewa na mashabiki wa R.O.M.A ambayo yamewashangaza wengi na kuvunja rekodi kwa muda mfupi ikiwa ni pamoja na kuwashukuru watanzania wote walioungana naye na kumfariji wakati wa matatizo.