Huduma za afya zazorota nchini Syria na kuleta shida kwa wananchi wake - MULO ENTERTAINER

Latest

7 Jan 2015

Huduma za afya zazorota nchini Syria na kuleta shida kwa wananchi wake

Sura ya Aleppo,ilivyo sasa.
Kikundi cha madaktari kutoka nchini Syria kimezishutumu nchi za Magharibi kwa kuwatelekeza raia kwenye suala zima la afya ,huku nchi hizo zikielemea zaidi katika suala la kutaka kuliangamiza kundi la dola ya Kiislam,IS.
Muungano huo wa matabibu kutoka Syria,umetoa tamko kwamba tangu nchi ya Marekani ilipoanza kuripua maeneo yanayoshikiliwa na wanamgambo hao wa dola ya kiislam nchini Syria kumekuwa na ongezeko la vifo kati ya thelathini hadi sitini kwa siku,zikiwa ni athari za vita hivyo .
Kikundi hicho kinaelekeza lawama zake kwa majeshi yanayomtii Rais Bashir al-Assad kwamba wanahusika kwa asilimia sabini hadi themanini ya vifo vya raia,na kusema kuwa dhamana ya pili ya vifo hivyo vya raia inaenda kwa kundi hila la dola ya kiislam kwa kuua raia wengi wasio na hatia.
Madaktari hao pia wameonya juu ya janga la kudorora kwa huduma za afya nchini Syria yakiwa ni matokeo ya miaka minne ya vita vinavyoendelea ,na Daktari mmoja kutoka mjini Aleppo ameshangazwa na idadi ndogo ya vituo vya afya huku akishuhudia kuwepo vituo vya afya vitano tu vinavyopaswa kuhudumia zaidi ya raia elfu tatu ambao wanakufa kutokana na magonjwa kama kipindupindu,homa za matumbo na kifua kikuu.