Wapiganaji wa Taifa la Kiislam (ISIS) wametoa picha za video ambapo wanatishia kuwaua mateka wawili wa Kijapan kama hawatalipwa Dola milioni 200 (Sh. Bilioni 358) katika muda wa saa 72 zijazo.
Mateka hao ni Kenji Goto Jogo mwandisi wa habari aliyekuwa anaandika kuhusu vita vya ndani vya Syria mwaka jana, na Haruma Yukawa mwanajeshi kutoka kampuni binafsi aliyekamatwa nchini Syria mwezi Agosti mwaka jana.
Tishio hilo limekuja baada ya Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, kuahidi kutoa kiasi hichohicho cha fedha kama msaada usiokuwa wa kijeshi kwa nchi zinazopigana dhidi ya ISIS.
Video hiyo iliyosambazwa katika tovuti zinazohusiana na wapiganaji hao, zilizomwonyesha mpiganaji mwenye lafudhi ya Kiingereza ambaye anajulikana kama ‘Jihadi John’ aliyeonekana katika video za mauaji ya kuwakata vichwa mateka David Haines, Alan Henning (Waingereza), na James Foley na Steven Sotloff (Wamarekani) hivi karibuni.
20 Jan 2015
New
Wapiganaji wa Taifa la Kiislam (ISIS) Wadai Fidia ya Dola Milioni 200 Kuwaachia Mateka wa Japan
mulo
News