MAJANGA..!! MUME AMKATA MDOMO MKE WAKE KISHA AJINYONGA KWA KUTUMIA GAUNI AKIMTUHUMU KUCHEPUKA NJE NDOA YAO - MULO ENTERTAINER

Latest

12 Feb 2015

MAJANGA..!! MUME AMKATA MDOMO MKE WAKE KISHA AJINYONGA KWA KUTUMIA GAUNI AKIMTUHUMU KUCHEPUKA NJE NDOA YAO

 

Mkazi wa kijiji cha Nyakabanga kata ya Butelankuzi, Bukoba vijijini, Eliud Charles (30) anadaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kutumia gauni la mkewe, Velidiana Eliud kutokana na wivu wa mapenzi.
 
Inadaiwa kabla ya kujinyonga jana saa 12 asubuhi, alimkata mapanga mkewe akimtuhumu kutembea nje ya ndoa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alisema wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu.
 
Inadaiwa baada ya kujibizana kwa maneno, mume alimkata mkewe sehemu za mdomo na mkono wake wa kulia.

 Kamanda Mwaibambe alisema mume aliingia ndani ya nyumba yake na kuchukua gauni la mkewe na kujining’iniza darini katika sebuleni ya nyumba yake.
 
Mwaibambe alisema Velidiana amelazwa katika Hospitali ya Ndolage wilayani Muleba na hali yake inaendelea vizuri.

 Mwili wa marehemu ulichukuliwa na ndugu zake na kuzikwa baada ya uchunguzi kukamilika.