Ni zaidi ya mara tatu kumekuwa na mijadala ndani ya Bunge la Tanzania tumesikia ikijadilia kuhusu njia ambayo itaweza
saidia kutafuta suluhu ya kudumu kwenye ishu ya tatizo la wanafunzi shule za Msingi na Sekondari kupata ujauzito.
Leo nimekutana na hii story nikajua kwamba kumbe tatizo hili sio la Bongo peke yake, Indonesia wao wameenda mbali zaidi, Jimbo la Java Mbunge mmoja alitoa pendekezo la kuwa na utaratibu wa kuwapima wanafunzi wa kike wanaomaliza shule za Sekondari kama wamewahi kukutana kimwili na wanaume, iwapo yoyote anakutwa kwenye hali kwamba aliwahi kukutana na mwanaume basi safari yake kimasomo itaishia hapo hatoruhusiwa kuendelea na masomo.
Ni nchi hiyo hiyo mwaka jana ilitoka ripoti ya utafiti iliyosema kumekuwa na zoezi la kupima hivyo askari wa kike na wanajeshi kitu ambacho kilikosolewa na watu wa haki za binadamu.
Viongozi wa dini pia walilaumu hilo japo walisema kuna dalili zote kwamba ishu hiyo imeendelea kufanywa chini chini kwa siri japo Serikali ilisisitiza kwamba haitoruhusu utaratibu huu kuwepo katika nchi hiyo.