Mpenzi Wangu Ananitaka Kinyume na Maumbile Nikiwa Katika Siku zangu - MULO ENTERTAINER

Latest

28 Feb 2015

Mpenzi Wangu Ananitaka Kinyume na Maumbile Nikiwa Katika Siku zangu

Dunia hii imejaa vituko jamani, kila ukisema kuwa umeona jambo la kituko unachodhania ni kikali zaidi, basi siku ijayo kinaibuka kingine kikubwa zaidi. Hebu soma mkasa wa dada Grace hapa chini halafu tusaidiane kumshauri

Dear Admin,
Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuendesha website hii, na umahiri wenu ndio umenisukuma leo hii nijitokeze hapa nikiomba ushauri kwa wasomaji wenu mahiri na wenye kustaarabika, maana huwa hakuandikwi mambo ya ajabu ajabu hapo.
Mimi ni binti mwenye umri wa miaka 24, nina mpenzi wangu ambaye hivi sasa tuna miezi takriban minne toka tuanze mahusiano yetu. Ni kijana mtanashati na mwenye kujimudu kwa upande wa kipato na kwakweli amekuwa msaada mkubwa sana kwangu na kwa familia yangu pale ambapo nimekuwa nikimshirikisha, ingawa sio sana kwasababu nami namiliki biashara zangu na zinanitosheleza kimahitaji ya lazima kwa ujumla.
Tatizo langu sasa kwa huyu mpenzi ni kuwa, yeye anapenda sana kushiriki tendo la ndoa. Yaani karibu kila siku yeye anataka tufanye hicho kitu na ikitokea siku hiyo anataka na niko kwenye mzunguko wa zile siku za wanawake, basi hunilazimisha tufanye hata kwa kutumia mpira. Tabia hii kwakweli imekuwa ikinikera sana, maana ni kama vile anataka kunitumia tu kama chombo chake cha starehe na wala sio kama mwenza wake na ninayehitaji pia kujaliwa.
Kilichonisukuma kuibuka kuomba ushauri leo hii ni kwamba, wiki jana nilikuwa kwenye siku zangu, na kama ilivyokuwa ada ya jamaa, akanijia siku hiyo akitaka tufanye mapenzi, mie nikamkatalia katakata maana nishaona namuendekeza sana, unajua alinijibu nini, eti “kama unaona unaumia kufanya hivyo ukiwa kwenye siku zako, basi uwe unanipa penzi kinyume cha maumbile” kha!!

Yaani niliishiwa nguvu, nikajiondokea zangu kwake na kwenda kwa rafiki yangu ambako niko hadi leo. Sasa najiuliza, huyu mwenzangu ana akili timamu kweli? Je, ananipenda au anataka kunitumia tu? Au ana ugonjwa fulani labda wataalamu wa tiba waniambie.
Natanguliza shukrani, naamini nitashauriwa juu ya hili.