Wema , Ivan and King Lawrenc |
“Yule ni...(tusi) ameniboa kweli...(tusi) unajua vitu vingine vya kipuuzi kabisa, wanatafuta kiki zisizokuwa za msingi wa...(tusi)” alisema Wema.Wema alisisitiza kuwa hataki kumzungumzia sana King kwani anaamini akifanya hivyo atamuongezea umaarufu ambao amekuwa akiutafuta muda mrefu.
King Lawrence amekuwa akimtusi Diamond mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii huku akionesha jeuri ya fedha kwa kile kinachoonekana kuumia kwake roho kwa kijana wa Tandale kumchukua shemeji yake Zari, aliyezaa na Ivan watoto watatu.