Mdau Henry Mdimu aanza harakati za kutoa somo kwa wauaji wa albino Thursday, 5 March 2015 - MULO ENTERTAINER

Latest

7 Mar 2015

Mdau Henry Mdimu aanza harakati za kutoa somo kwa wauaji wa albino Thursday, 5 March 2015




Balozi wa Imetosha,Henry Mdimu (kati) azungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati azungumzia harakati zake za kutaka kwenda kanda ya Ziwa ili kuihamasisha jamii juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.Kulia ni Mwenyekiti wa Imetosha Movment,Masoud Ali "Kipanya" na kushoto ni Monica Joseph mjumbe wa Imetosha. 

Balozi wa Imetosha,Henry Mdimu amewataka watu wajitokeze katika harakati za kupambana na watu wenye imani potofu za kuwaua watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino). 


Mdimu amesema uchunguzi umebaini ukosefu wa elimu kwa watu wenye imani hizo ndiyo hupelekea mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi hivyo silaha ya elimu ni sehemu kubwa ya harakati hapa nchini. 


Hayo ameyasema leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kusema kuwa ana mpango wa kwenda kanda ya Ziwa ili kuihamasisha jamii juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi. 


Aidha,Mdimu ameahidi kutoa elimu hiyo kwa njia ya sanaa kwa kuwatumia baadhi ya wasanii kama Jhikoman,Kassim Mganga,Profesa J,Ray C,Fid Q,Roma Mkatoliki pamoja na Dami Msimamo. 


Pia amevitaka Vyombo vya Habari kutoa ushirikiano katika harakati hizo za kuhakikisha wanatokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi. 



Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni Wajumbe wa Imetosha,Joachim Mushi akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo. 

Baadhi ya Wajumbe wa Imetosha wakiwa kwenye picha ya pamoja.