Lugola Awajia Juu Wanaoshangaa Mtuhumiwa Kufia Mikononi mwa Polisi - MULO ENTERTAINER

Latest

13 Sept 2018

Lugola Awajia Juu Wanaoshangaa Mtuhumiwa Kufia Mikononi mwa Polisi

Lugola Awajia Juu Wanaoshangaa Mtuhumiwa Kufia Mikononi mwa Polisi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amekemea vikali tabia ya Wananchi kujichukulia hatua mkononi na kwenda kuchoma vituo vya polisi pindi yanapotokea matatizo ya vifo vya watuhumiwa wakiwa mikononi mwa polisi, huku akieleza kuwa kifo ni mtego mtu atakufa sehemu yoyote ile hata akiwa anafanya mapenzi.



Waziri Kangi amefunguka hayo leo Septemba 13, 2018 Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji aliyehoji mahabusu kufia mikononi mwa polisi.