Michuano ya UEFA kushika kasi leo, nimekuwekea ratiba hapa. - MULO ENTERTAINER

Latest

10 Mar 2015

Michuano ya UEFA kushika kasi leo, nimekuwekea ratiba hapa.

Michuano ya marudiano ya hatua ya 16 bora katika UCL yatarajiwa kuanza leo.
Timu mbili za kwanza zitakazoingia robo fainali ya mashindano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya zinatarajiwa kubainishwa leo.
Mabingwa watetezi Real Madrid walioibuka na ushindi wa magoli 2 – 0 ugenini dhidi ya Schalke 04 katika mechi ya kwanza wanatarajia kujihakikishia tiketi ya robo fainali. Schalke 04 nayo itakuwa na kibarua kigumu cha kuipindua Real Madrid.
Kwingineko, timu ya Porto itawakaribisha Basel nyumbani katika mechi itakayobainisha mshindi atakayeingia robo fainali baada ya kutoka sare ya 1 – 1 katika mechi ya kwanza.
Mechi hizo zinatarajiwa kuanza mwendo wa saa 21.45 usiku kwa nyakati za Uturuki.