HALI si shwari ndani ya klabu ya Azam baada ya uongozi wa klabu hiyo kumtupia virago kocha wake mkuu Mcameroon Joseph Omog.
Mbali na Omog, mwingine aliyetupiwa virago ni msaidizi wake namba mbili Ibrahim Shikanda raia wa Kenya.
Habari za uhakika kutoka ndani ya uongozi waAzam zimesema Omog na Shikanda wamefutwa kazi kutokana na mwenendo mbaya wa timu kwenye michuano ya kimataifa na ile ya Ligi.
Azam imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2 na El Merreikh ya Sudan. Katika mechi ya kwanza iliyofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi Azam ilishinda mabao 2-0, lakini ikafungwa mabao 3-0 katika mechi ya marudiano iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Khartoum Sudan.
“Kocha amefutwa kazi kwani uongozi umeona hastahili kuendelea kuifundisha Azam, hana mbinu za ushindi, tangu achukue timu imekuwa ikifanya vibaya sasa yeye na Shikanda wamefukuzwa na timu itakuwa chini ya kocha msaidizi Mganda George Nsimbe ,” alisema mtoa habari wetu.
Azam pia ambayo ndiyo bingwa mtetezi wa Ligi Kuu bara, haifanyi vizuri licha ya kushika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 27, lakini imekuwa ikipata ushindi kwa tabu katika mechi zake.
Omog aliyeanza kazi Desemba 2013 akichukua mikoba ya Stewart Hall kutoka Uingereza ameiongoza Azam katika mechi 55 kwenye michuano yote ambapo imeshinda mechi 30, imetoka sare mara 14 na kupoteza mechi 11.
Aidha ikiwa chini yake, Azam ilitwaa taji la Ligi Kuu kwa mara ya kwanza Mei mwaka jana.