Tanzania tuliivamia DRC kuwatoa M23 mbona kigugumizi kuwang'oa Alshaabab? - MULO ENTERTAINER

Latest

13 Apr 2015

Tanzania tuliivamia DRC kuwatoa M23 mbona kigugumizi kuwang'oa Alshaabab?

Nimekuwa nikishawishi serikali yetu mara kadhaa kuwa kuna haja ya Tanzania kuivamia Somalia kijeshi kwa kushirikiana na majeshi mengine ya Afrika yaliyoko Somalia ili kuwang'oa Alshaabab.

Kuna haja ya sisi watanzania kufanya hivyo kwani kwa sasa ni dhahiri ndugu zetu wa Kenya wanakaribia kuzidiwa nguvu na hawa alshaabab.

Ikumbukwe wakati alshaabab wanaanza harakati zao walikuwa wanateka meli tu ambazo zilikuwa zinapita pwani ya Kenya na Somalia na kuteka watalii kisha kutoa rai ya kubadilishana mateka na fedha.

Kwa sasa wamejipanua na kutaka kuanzisha jamuhuri yao hivyo kuwa tishio zaidi huku wakijipambanua kwa mgongo wa uislamu!

Na endapo wakiachwa watawale kama wanavyofanya sasa baada ya muda pwani nzima ya Afrika mashariki haitokuwa salama tena.

Kuna vitisho kadhaa ambavyo hufanya alshaabab endapo unaenda kwenye ardhi yao kuwapiga kama vile kutoa maneno ya vitisho, kufanya mashambulizi ya kushtukiza kwa raia na kutesa wanajeshi wanaowakamata/kuwateka.

Mfano, Marekani ilipoivamia Somalia kuwapiga alshaabab, kwa bahati mbaya alshaabab wakamkamata askari mmoja wa Marekani, wakamuua kikatili kisha kuanza kumburuza akiwa amefungwa nyuma ya gari mitaani Mogadishu. Baada ya kuona tukio lile raia wa Marekani wakapiga makelele serikali yao iwaondoe askari walioko Somalia. Kweli askari wengi wakarudishwa Amerika. Kitisho kile kikawa kimefanikiwa.

Wametoa vitisho pia mara kadhaa kwa serikali ya Kenya na Uganda kwa kuwavamia na kuua raia wao mara kadhaa kama ile ya westgate, Garissa, nk.

Tusiogope vitisho tuna jeshi imara ambalo halina shaka na tumelipa sifa kila uchao.

Twendeni Somalia!!