Dudu Baya 'Siwezi Kufanya Kazi na Mr Nice Mpaka Pale Atakapo Badilika' - MULO ENTERTAINER

Latest

6 May 2015

Dudu Baya 'Siwezi Kufanya Kazi na Mr Nice Mpaka Pale Atakapo Badilika'

Rapper mkongwe, Dudu Baya amesema kwa sasa amekuwa rafiki mkubwa na aliyewahi kuwa hasimu wake, Mr Nice na kuweka nia yake ya kufanya naye kazi ya pamoja.

Dudu amesema hayo alipoongea na Enewz ya EATV na kuongeza kuwa mpaka sasa kinachochelewesha collabo kati yao, ni mtindo wa muziki wa TAKEU ambao Nice anaufanya.

“Unajua naweza kuingia studio kufanya ngoma na Nice endapo atabadilika na tukafanya rekodi yenye mahadhi mengine kutokana na msimamo wangu mimi siwezi kunengua hata siku moja,” amesema.