Rais Kikwete Apiga Mkwala Asema Hatakubali Misaada Yenye Masharti Kuyumbisha Nchi - MULO ENTERTAINER

Latest

21 May 2015

Rais Kikwete Apiga Mkwala Asema Hatakubali Misaada Yenye Masharti Kuyumbisha Nchi

Rais Jakaya Kikwete amesema nchi yake haitakubali kuyumbishwa na wahisani ambao kila mara wamekuwa wakitishia kusitisha misaada yao kama mambo wanayoyataka yafanywe na serikal hayatafanywa na kuwataka wahisani wenye tabia hiyo kuacha kutumia misaada yao kama fimbo ya kuichapa Tanzania na kama wataendelea kufanya hivyio ipo siku itaikataa hiyo misaada.

Mh Kikwete ameyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa mpango wa uendeshaji wa shughuli za serikali kwa uwazi yaania Open Govermnent Partineship –OGP ambapo amesema serikali nayo inahadhi yake na siyo kila jambo kuburuzwa.

Kuhusu uendeshaji wa serikali Mh Kikwete amesema wananchi wanapaswa kujua namna shughuli zinavyokwenda ili waweze kuhoji pale mambo yanapokuwa kinyume na matarajio yao.

Kwa upande wake waziri wa nchi ofisi ya rais utawala bora Mh George Mkuchika amesema tangu Tanzania ingiye katika mpango huo wa OGP mambo mengi ya serikali yamekuwa hadharani na hivyo kuwafanya wananchi wengi kujua namna serikali inavyofanya mambo yake.

Naye mkurugenzi wa Twaweza Aidan Eyakuze amesema jambo muhimu ambalo viongozi wa Afrika wanapaswa kujua ni kwamba wanapaswa kuheshimu utawala wa sheria nakuruhusu uhuru wa mawazo huku akiomba serikali ya Tanzania kuangalia upya sheria yake
ya takwimu na mtandao ili kuweza kutoa fursa kwa watu wengi kutoa mawazo yao.