Zari wa Diamond Ateswa na Picha Inayoonyesha Akiwa Beneti na Pedeshee Katunzi - MULO ENTERTAINER

Latest

23 May 2015

Zari wa Diamond Ateswa na Picha Inayoonyesha Akiwa Beneti na Pedeshee Katunzi


MCHUMBA wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’,  Zarina Hassan ‘Zari’ amedaiwa kuangua kilio baada ya kuvuja kwa picha yake na mfanyabiashara maarufu jijini Dar, Mzamili Katunzi ambayo ilidaiwa kuwa ni mtu wake na kusababisha gumzo mjini.

Mtu wa karibu na Zari amefunguka kuwa Zari alijisikia vibaya sana baada ya kuona picha hiyo na kukasirika hivyo kuanza kuwasaka watu walioivujisha kwani walikuwa na nia mbaya ya kumgombanisha lakini wamechemka.
Zari kamaindi kweli, anajiuliza huyo aliyeivujisha alikuwa na lengo gani?” alisema mtu huyo

Jitihada za kuzungumza na Zari hazikuzaa matunda lakini bahati nzuri Diamond alipatikana na kufafanua:
 “Ni kweli zimemsumbua baby lakini nimemuweka sawa kwa kuwa najua ni mambo ya mitandao, hakuna ukweli wowote.”