Wapelelezi wanaofatilia kashfa ya rushwa inayohusu shirikisho la soka ulimwenguni FIFA wameahidi kufichua makubwa zaidi baada ya kugundua siri nzito zilizojificha kwenye mchakato wa kuchagua mwenyeji wa kombe la dunia.
Wapepelezi hao wakiongozwa na Mwanasheria mkuu wa Uswisi, Michael Lauber wamesema kuwa kuna matukio karibu 53 ya uchakachuzi na utakatishaji haramu wa fedha ambayo yamegundulika kwenye michakato tofauti ya kumpata mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia na matukio haya yamehusishaa watu wazito ambao kama yatagundulika undani wake yatazua hofu na utata mkubwa.
Mwanasheria huyo ameonya kuwa hatajali kama upelelezi wake utasababisha hasara ya fedha au kupokonywa uwenyeji kwa nchi za Urusi na Qatar na anachojali ni ufanisi wa kazi yake na si kitu kingine.
Imedaiwa kuwa upelelezi huu unahusisha kuhojiwa kwa viongozi wa juu wa FIFA akiwemo rais wa zamani Sepp Blatter ambaye hivi karibuni alitangaza kujiuzulu siku chache baada ya kuchaguliwa kwa kipindi cha tano.
Rais wa Fifa wakati akitangaza mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 .
Rais wa FIFA wakati akitangaza mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 .
Viongozi kadhaa wa zamani wa FIFA wakiwemo Mmarekani, Chuck Blazer na rais wa zamani wa chama cha soka cha Trinidad and Tobago, Jack Warner wameahidi kutoa ushirikiano kwa wapelelezi huku wakiahidi kuwa watazungumza bila kuficha.