Mchezaji Lionel Messi Amulikwa na Kitu cha Hatari Akiwa Uwanjani..Check Picha za Tukio zima Hapa - MULO ENTERTAINER

Latest

28 Jun 2015

Mchezaji Lionel Messi Amulikwa na Kitu cha Hatari Akiwa Uwanjani..Check Picha za Tukio zima Hapa

Messi na timu yake ya taifa wamefanikiwa kuingia nusu fainali ya Copa America hayo tuliyajua baada ya mechi kuisha, tuliyoyajua leo ni kuhusu Messi kumulikwa na kitu cha kijani ambacho kitajwa kama “green laser” ambapo miale hiyo ilipiga sehemu ya mbele ya kichwa chake.

Wachambuzi wanasema hiyo miale inaweza kutoka kwenye kitu kinaitwa laser pen ambapo lengo lao ni kumulika usoni Messi na kumtoa kwenye mchezo au kumzozoa tu usoni. Kwenye historia inasemekana sio mara ya kwanza kwa Messi kufanyiwa hivyo, hata Ulaya kuna wahuni wanaofanyaga hivyo.

Umbo la laser pen ni kama peni ya kawaida kwa hiyo hata sehemu ya kusachiwa sio rahisi kujua ukubwa wa matumizi zaidi ya pen hiyo. Ushahidi wa miale hiyo umeonekana kwenye picha zilitoka mtandao hivi sasa