Wastara |
Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni, Wastara alisema kuwa kwa sasa wao watakuwa lulu kwa wanasiasa na kutumiwa ipasavyo lakini baada ya mchakato wa uchaguzi kuisha wataonwa hawafai, kitendo ambacho si kizuri kwani wanatakiwa kukumbukwa wakati wote.
- “Yaani kuna wakati sipendi kabisa siasa na wala sipendi kufungamana na mtu kwa sababu nilichojifunza sisi wasanii tunatumiwa kama Big G tu kwa sasa kwa sababu wana shida, baada ya hapo tutaachwa solemba na hata tutakapohitaji kusaidiwa jambo lenye masilahi kwetu tutaonekana wasumbufu,” alisema Wastara.