Aunt Lulu Awashangaa Wanawake Wanaomkosoa - MULO ENTERTAINER

Latest

8 Jul 2015

Aunt Lulu Awashangaa Wanawake Wanaomkosoa

Mtangazaji na muigizaji wa filamu hapa Bongo, Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’ amewashangaa wanawake  wote  ambao  wamekuwa wakimtukana kila anapoweka picha zenye mikao ya kihasara kwenye mtandao ya kijamii na kusema endapo wataendelea atawachukulia mabwana zao.

Akizungumza na Tanuru la Filamu, Aunt Lulu alisema kwamba wanawake ndiyo wanaongoza kumtukana kila akiweka  picha za kuonyesha  jinsi  Mungu alivyolia kumuumba  na kumpa  mapaja yenye ushawishi  kwa kila anayeyaangalia awe wa kike ama wakiume.

“ Mungu amenijalia akuwa  na hips nzuri , makalio makubwa na muonekano mzuri  kwa  watu sasa kwa nini wananitukana  kana kwamba ninawabebea mabwana zao  na  endapo wataendelea nitafanya hivyo ili waseme vizuri  kwani  nimechoka kusemwa kwani nina uhuru  wa kuweka picha yoyote ilimradi haivunji maadili ya Kitanzania,” alisema Aunty Lulu.

Alisema kamwe hataacha  kufanya  hivyo kwani  yupo huru  na  anajua nini anakifanya  na si kuongozwa na  watu tena wanawake wenzake  ambao kwa kiasi kikubwa  wamejaa wivu kuliko wanaume.