Basi la Sabuni Express limegongana na gari la Kanisa Katoliki. Ajali imetokea Bugorora Kyaka Wilayani Misenyi. - MULO ENTERTAINER

Latest

28 Jul 2015

Basi la Sabuni Express limegongana na gari la Kanisa Katoliki. Ajali imetokea Bugorora Kyaka Wilayani Misenyi.



Ajali mbaya imetokea eneo la Bugorora Kyaka leo, inahusisha Basi la kampuni ya Sabuni lililokuwa likitokea Karagwe na Land Cruiser ya Kanisa.

Taarifa za hawali zinasema watu si chini ya watano wamepoteza maisha kwenye eneo la tukio.

Basi la Kampuni ya Sabuni linalofanya safari kati ya Kagera na Mwanza limegongana na gari ndogo aina ya Land Cruiser iliyokuwa na mapadre na masista katika eneo la Bugorora nje kidogo ya Kyaka wilayani Misenyi mkoani Kagera.

Basi hilo nambari za usajiri T650 BFI na Cruiser T166 AGU ambapo waliotajwa kupoteza maisha kwa taarifa za awali ni Padre Onesmo Kahabwa na Michael Mwelinde pamoja Sista Magret Tadebe ambao ni wa Parokia ya Katoke waliokuwa wakitokea Rulenge wilayani Ngara.