Kama Lowassa ni Fisadi, Rais Kikwete tamka Hadharani - MULO ENTERTAINER

Latest

4 Jul 2015

Kama Lowassa ni Fisadi, Rais Kikwete tamka Hadharani

Kama Lowassa ni fisadi na mwizi wa mali za watanzania.

Mwenyekiti wa CCM JK simama hadharani na utamke wazi wazi la sivyo tunaposema CCM ni chama cha mafisadi kwa miaka yote msipingane na Sisi.

Au La na mwenyekiti wa CCM utakuwa upo kwenye cheni moja na EL
Mnaogopa nini kumtaja kama ni fisadi?

Na kwanini mtumie vijana wa ngazi za chini kama Makonda na Nape kwenye chama chenu kumwandama na nyie mkiwa kimya?

Tunaitaji matamko ya
1.Mwenyekiti wa CCM
2.Makamu mwenyekiti CCM
3.Katibu Mkuu CCM

Sio Mavuvuzela wa chama,la sivyo nyote ni mafisadi na wezi tu mnaooneana aibu kwa kuzidiana ufisidi.