Kwanini Diamond Alishinda: Tofauti za Wazi na za Msingi Kati ya KTMA na MTV Awards! - MULO ENTERTAINER

Latest

20 Jul 2015

Kwanini Diamond Alishinda: Tofauti za Wazi na za Msingi Kati ya KTMA na MTV Awards!

Maoni Huru Kutoka Kwa Ndau Anaitwa  Matumbo Huko Jamii Forums
Jisomee Mwenyewe Hapa Chini:



Toafauti ya kwanza kabisa, inayotofautisha kati ya KTMA na MTV Awards ni kwamba, kwa KTMA, msanii ana uwezo wa kutoka na kontena moja la tuzo peke yake na kwa wakati mmoja wakati kwa MTV ni ndoto kufanya hivyo! Hadi sasa, msaniii anayeongoza kutoka na kontena la tuzo za KTMA kwa wakati mmoja ni Diamond Plutnumz ambae aliibuka na tuzo 7 kisha wanafuatia Ali Kiba na 20% ambao kila mmoja amepata kuibuka na tuzo 5.

Ukweli huo hapo juu unatokana na tofauti za kimsingi zinazounda Tuzo za KTMA na MTV ambazo ni:
>>>Wakati MTV Awards inakutanisha wanamuziki MAHIRI kutoka majiji makubwa kabisa barani Afrika kama vile Dar es salaam, Nairobi, Lagos, Johannesburg, Cape Town, Accra, Kinshasa n.k, KTMA kwa kiasi kikubwa inakutanisha wasanii kutoka kaeneo kadogo tu duniani kanakoitwa Wilaya ya Kinondoni!
>>>Tofauti na MTV Awards, pia MC wa KTMA most likely atatoka wilaya ya Kinondoni, wakabidhi tuzo watatoka huko huko, venue, wilaya ya Kinondoni… tumeenda mbali sana, Wilaya ya Ilala! Majority ya watakaopita Red Carpet-- wilaya ya Kinondoni, watakaokuja kuburudisha, majority watatoka wilaya ya Kinondoni and, to cut story short, almost everything, for KTMA kitakuwa ni Wilaya ya Kinondoni!
>>>Wakati host mkubwa wa KTMA ni wilaya ya Kinondoni na kidogo Ilala na hivyo kuzifanya tuzo za KTMA kuwa ni tuzo za WA HAPA HAPA, hosts wa MTV Africa Awards wanakuwa nchi mbalimbali!! Hawa WA HAPA HAPA wasubirie host city awe Dar es salaam ndipo labda waje kuambua kama ambavyo Wakenya walipata kuzizoa mwaka 2009 baada ya Host City kuwa Nairobi!!!
>>>Wakati kwenda kwenye tuzo za MTV, majority ya wasanii watatakiwa kuchukua air flight, kwa KTMA, in fact, hata kupanda gari ni mbwembwe coz’ majority ya wasanii wana uwezo wa kufika kwenye venue hata kwa Bajaj simply because Tuzo zenyewe zinakutanisha WA HAPA HAPA!!!
>>>Wakati MTV Awards inakutanisha wasanii wanaofanya kazi zao kwa lugha mbalimbali za kimataifa kama vile Kiingereza, Kifaransa, Kireno n.k, KTMA, kwa kiasi kikubwa, inakutanisha Wamatumbi peke yao, kwa maana ya watumiaji wa Lugha ya Kiswahili kwa kuwa ni tuzo za WA HAPA HAPA!

Dah! Tofauti zipo nyingi sema wakati ukuta! Je, ewe mwenzangu unaweza kutaja tofauti zingine za WAZI (sio za KIUFUNDI) kati ya MTV Awards na Kinondoni Tanzania Music Awards?

Hata hivyo, kabla sijakusanya kila kilicho changu na kusepa wacha niseme jambo moja! Nimeona watu hapa eti wanaponda Tuzo ya Best Live ACT na kufananisha na suala la kukata mauno! Short and clear, ukitoa hiyo hoja mbele ya watu wanaoifahamu tasnia ya muziki moja kwa moja watakauona muziki huufahamu! Ingekuwa Live Act ni kukata mauno basi hizo tuzo kila mwaka, sio Afrika tu bali hata duaniani zingeenda DRC!!

Biashara ya muziki duniani imebadilika sana, mauzo ya CDs sio deal tena kwa wasanii! Africa ambako hata masuala ya hati miliki ni hovyo, ukiacha endorsement wasanii wanategemea zaidi performance jukwaani na kupitia hili eneo, ndipo pekee msanii kwa kiasi kikubwa anaweza kuwa na uwezo wa kuuza kazi au bidhaa zake zingine inculding hizo CD kwa kuwa fans wako wanakuwa wamekusanyika sehemu moja kuliko kuwataraji kwamba wataenda dukani kununua CDs zako au nguo zako!! Live Act ni eneo lenye faida na mzunguko mkubwa wa pesa pengine kuliko eneo lingine kwenye biashara ya muziki na ndio maana, leo hii tukiambiwa mathalani Lady Gaga anakuja Dar, basi Dar mzima itakuwa full vurugu; kuanzia promotions kwenye medias, maandalizi ya venue, deals za kuuza ticket, kampuni kubwa kutaka kudhamini na kadhalika bila kusahau mzunguko wa pesa utakaotokea kwa wauza vinywaji na chakula!! Huko kote, ni mzunguko wa pesa … watu watapanda magari kutoka hata Mwanza kuja Dar es salaam only for Live Act! Kwahiyo ni kichekesho mtu akisema this’s all about kukata mauno! Mauno yanakatwa kitandani, jukwaani is all about performance, nyie watu wa wapi!!!

In short, kwenye Best Live Act wanaangalia pamoja na mambo yafuatayo:
>>>ENERGY: Kuwa Mkata Mauno Bora kuliko wote duniani lakini kama hauna ENERGY, pisha wenye pumzi wafanye kazi yao!
>>>CROWD ENGAGEMENT: Kuwa na pumzi za kutosha lakini ikiwa hauna uwezo wa kushirikisha crowd na kuleta shangwe kwenye show, please, pack and go because you’re not BEST LIVE ACT
>>>BEST MUSIC: Huwezi kuwa na muziki wa hovyo halafu ukaota kuwa Best Live Act unless kama ni kwenye hizi tuzo za WA HAPA HAPA!! Huwezi kuwa na crowd engagement or crowd feedback wakati muziki wako ni mbovu unless kama ni kwenye hizi tuzo za WA HAPA HAPA! ​

Halafu mwambieni jamaa, haya mambo mi natembelea kwenye akaunti yake halafu ananiambia nisiue tembo wakati hata Mikumi sijawahi kufika isn't fair at all... huu ni uonezi wa wazi wazi! Yaani mie nimetulia zangu tuli na ka-Techno kangu halafu unaniambia nisiue tembo?