Mrembo Akuhumiwa Jela Kwa Video Tata Mtandaoni - MULO ENTERTAINER

Latest

28 Jul 2015

Mrembo Akuhumiwa Jela Kwa Video Tata Mtandaoni

Mnenguaji wa kike nchini Misri, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa la kuonekana kwenye video yenye utata mtandaoni.

Hukumu hiyo imetolewa na mahakama moja nchini humo kwa kosa la kuchochea ngono baada ya kuonekana katika video yenye utata katika mtandao.

Mrembo huyo aliyetambulika kwa jina la Reda al – Fouly alitiwa mbaroni, mara baada ya video hiyo ya miondoko ya Pop kuoneshwa hadharani na baadaye kudhihakiwa kuwa imeenda kinyume na tamaduni za kiarabu.

Muimbaji huyo wa kike alitakiwa kufafanua mavazi -aliyoyava kwenye wimbo unaoitwa Sib Eddi au let it go of my hand.

Hata hivyo inadaiwa kuwa mkurugenzi wa video hiyo, Wael Seddiki , aliondoka nchini Misri wakati wimbo huo ulipoanza kupondwa kwenye mitandao ya kijamii ili kukwepa lolote ambalo lingeweza kutokea..

Video  Yenyewe  Iko  Hapo  Chini