Producer Manecky na Diamond Platnumz Wamaliza Tofauti zao, Waamua Kufanya Kitu Hichi Pamoja - MULO ENTERTAINER

Latest

9 Jul 2015

Producer Manecky na Diamond Platnumz Wamaliza Tofauti zao, Waamua Kufanya Kitu Hichi Pamoja

Mtayarishaji wa muziki wa AM records, Manecky na Diamond Platnumz wamemaliza tofauti zao.

Manecky ameiambia Bongo5 kuwa ameanza kurekodi tena na Diamond baada ya miaka takriban miwili ya kutofanya kazi pamoja.

“Unajua kuna mzingira fulani yalijitokeza kati yangu mimi na Diamond tukawa muda mrefu sana hatujaongea na kuonana na kufanya kitu,” mtayarishaji huyo ameiambia Bongo5.

“Unajua kuna time inafika kila mtu anagundua ana mapungufu yake, sasa mnapoamua kuachana na mambo hayo mnaachana nayo. Sasa mimi sioni kama kuna sababu ya kukaa tena chini na kumuangalia nani alikosea. Sasa hivi tunasonga kwenda mbele, sasa hivi tupo fresh ndio maana tumeshaanza kurekodi ngoma mpya na Nay wa Mitego ili kutengeneza kitu kizuri,” ameongeza Manecky.

Hata hivyo Manecky amesema bado anapata wakati mgumu kuitafuta chemistry yake na Diamond kwakuwa ni kipindi kirefu hawajafanya kazi pamoja.

“Sasa hivi napata wakati fulani mgumu, unajua tumekaa muda mrefu hatujaonana wala kuongea/ Utajikuta unafanya kazi kwa mazingira fulani ili upate kitu kizuri ili kazi iwe nzuri.”