Staa wa Bongo Fleva alieanzia uigizaji, Snura Mushi amedaiwa kufunga ndoa ya siri na mchumba wake wa siku nyingi ambaye pia ni mzazi mwenziye,DJ maarufu mjini Mbeya,Hunter.
Habari zinasema kuwa katika sherehe ya ndoa hiyo walialikwa watu wachache kutoka kwenye pande mbili za familia ya wanandoa hao na ilifungwa kwa siri jijini Dar.
Kupitia U heard na Soudy Brown amezungumza na Snura ambaye amekana kufunga ndoa,lakini alipoulizwa kama aliweza kuficha mimba hadi alipojifungua je? Hawezi kuficha kufunga ndoa?
‘’Jamani sijafunga ndoa kama nimefunga muulize mpenzi wangu Hunter au meneja wangu HK,’alisema Snura.
Hata hivyo Hunter alipoulizwa kuhusu suala hilo alijibu kwa ufupi kuwa hajafunga ndoa na Snura.