‘You Are so Pretty’, ni Kauli ya Jay Z Alipomuona Vanessa Mdee - MULO ENTERTAINER

Latest

8 Jul 2015

‘You Are so Pretty’, ni Kauli ya Jay Z Alipomuona Vanessa Mdee

Vanessa Mdee anaweza kumfanya Beyonce anune au apate wivu kwakuwa muimbaji huyo wa ‘Nobody But Me’ aliwahi kulivutia jicho la rapper mwenye nguvu zaidi duniani, Sean Carter aka Jay Z.

Akiongea kwenye kipindi cha Chill na Sky, Vanessa alisema yeye mwenyewe alipokuna na rapper huyo wa ‘Run This Town’, mdomo wake ulipigwa ganzi kwa muda na maneno kushindwa kumtoka.

“Ooh my God! I was so nervous,” alikumbushia Vanessa.

“Lakini bahati nzuri nilikuwa sim-interview. Halafu mimi nina ugonjwa fulani hivi, kama nampenda mtu au nam-admire mtu nanayamazaga kimyaa,” aliongeza Vanessa.

“I was just like…. And he was so nice, he was like ‘ooh my God you’re so pretty’, like ‘they had to put your face on MTV’. I was like ooh my God ataniua…sasa sijui hata jinsi ya kujibu ni kama lugha inanipotea.”

Vanessa alidai kuwa Baba Blue Ivy ni mtu poa tofauti kabisa na watu wanavyomchukulia.

“He was so nice, very calm. Nikamkumbusha kwamba walikuja Tanzania… and he was like ‘yeah Tanzania is a beautiful country’. Yaani very nice guy, very diplomatic. Halafu hana majidai ya ajabu, labda kwa sababu mimi nilikuwa back stage and there was nobody in backstage,” alieleza Vee Money.